Kituo cha Taarifa
za Maendeleo Tanzania (TDIC) kumefunguliwa
rasmi na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Ndugu
Marten Lumbanga, katika tafrija iliyoandaliwa
kwa pamoja na wadau mbali mbali. Kituo hiki
kimefunguliwa na serikali pamoja na wadau
mbalimbalii kwa ajili ya kukusanya na kusambaza
taarifa za maendeleo ya Tanzania kutoka
kwa wadau mbalimbali kwa njia ya maandishi
na electron.
Pia kituo kitakuwa sehemu ya kupatikana
kwa taarifa za kazi za maendeleo zinazoendeshwa
na Wahisani na kuchochea ukuaji wa maarifa
kwa shughuli za mandeleo ya Tanzania.
Kituo kinahudumia wateja wafuatao: wahisani
wa maendeleo, watendaji wa serikali,wasomi,
sekta binafsi, mashirika ya kidini n.k.
|