| |
Kituo cha Habari
za Maendeleo Tanzania ni kituo kinachotoa
huduma za marejeo kilicho wazi kwa umma
wote unaohitaji taarifa kuhusu maendeleo
nchini Tanzania, hususani watoa maamuzi,
wanataaluma, waandishi wa habari, wanasiasa,
vijana na watafiti.
Kituo pia huendesha majadiliano mbalimbali
kwa ajili ya maendeleo na mada zinazohusiana
na maendeleo katika ukumbi wake wa majadiliano
uliosheheni vifaa vya kisasa vya kuendesha
mikutano.
Machapisho katika kituo yanaweza kupatikana
kwa mtandao na kwa kutumia programu ya katalogi
kwa ajili ya kupata kwa urahisi machapisho
yaliyopo.
Kutumia Mtandao
Huduma ya mtandao kwa kutumia kompyuta za
kituo inatolewa kwa umma ili kupata taarifa
za maendeleo, kazi mbalimbali na taarifa
nyingine zinazohitajika kwa ajili utafiti
|